Jumanne 6 Oktoba 2026 - 22:20
Ujumbe wa Mufti wa Yemen kwa Sheikh Al-Khatib; Wanazuoni Duniani wakabiliane na Madai ya Saudi Arabia Dhidi ya Matakatifu

Hawza/ Ujumbe wa Mufti wa Yemen kwa Sheikh Al-Khatib; ujumbe huo umetolewa katika wito wa kuwakusanya wanazuoni wa duniani ili kukabiliana na madai ya Saudi Arabia dhidi ya matakatifu.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika juhudi zinazoendelea za kuweka wazi msimamo wa Yemen kuhusu tuhuma zinazorudiwa mara kwa mara na Saudi Arabia dhidi ya matakatifu ya Umma, ujumbe kutoka kwa Mufti Mkuu wa Yemen, Sheikh Shamsuddin Sharafuddin, uliwasilishwa kwa Sheikh Ali Al-Khatib, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon, na ujumbe huo uliwasilishwa na ujumbe wa Yemen wakati wa ziara yao nchini Lebanon.

Katika ujumbe huo, aliombwa kuufahamu ujumbe wa wanazuoni wa Yemen, na kushiriki katika kuusambaza na kuweka wazi ukweli wa msimamo wa Yemen katika kukabiliana na madai ya Saudi Arabia kwamba Makkah Tukufu na maeneo matakatifu yanalengwa.

Aidha, katika barua hiyo, wanazuoni wa Umma wameombwa kushiriki katika kukanusha upotoshaji huu na kuweka wazi ukweli mbele ya maoni ya umma katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa upande mwingine, Sheikh Al-Khatib alisema katika hotuba yake mbele ya ujumbe huo: “Tunasikitishwa na yanayoendelea nchini Yemen, yaani vita ambavyo vimeendelea kwa zaidi ya miaka 11, mzingiro ambao umewekwa dhidi ya watu wa Yemen, na mapambano yanayoendelea.”

Aliongeza: “Ilipaswa mapambano haya yawe dhidi ya adui ‘Musraeli’ na dhidi ya maadui wa Umma, wala si baina ya wana wa Umma wenyewe.”

Sheikh Al-Khatib pia alieleza matumaini yake kwamba: “Nguvu na juhudi zote zielekezwe kwenye suala kuu, yaani suala la Palestina, na katika kukabiliana na adui ‘Muisraeli’ mwenye kiburi ambaye anawatishia Waarabu na Waislamu wote.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha